Date:
22-12-2025
Reading:
Mithali 21:28-31
Hii ni Advent
Jumatatu asubuhi tarehe 22.12.2025
Mithali 21:28-31
28 Shahidi wa uongo atapotea; Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo.
29 Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu; Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake.
30 Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya Bwana.
31 Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini Bwana ndiye aletaye wokovu.
Tutazamie kwa furaha ujio wa Mwokozi;
Tunasoma sehemu ya Mithali za Suleimani kuhusu yapasayo wanadamu katika maisha ya kila siku. Leo Suleimani anazuia waaminio kuwa mashahidi wa uongo, anawasihi waaminio kuwa na njia nyoofu mbele za Mungu. Anapendekeza hekima na ufahamu juu ya Bwana akihitimisha kwamba Bwana ndiye aletaye wokovu.
Somo linaonesha kuishi inavyofaa kwa kila aaminiye. Yaani Suleimani anatoa ujumbe kwa waaminio kwamba waishi vipi. Yametajwa machache kutukumbusha kutenda yafaayo kama hayo, ili Yesu Kristo tunayemngojea kurudi kwa mara ya pili asituache kwenye ufalme wake. Amina.
Tunakutakia maandalizi mema ya sherehe za Noeli.
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
