Date:
18-09-2025
Reading:
1Yohana 4:19-21
Alhamisi asubuhi tarehe 18.09.2025
1 Yohana 4:19-21
19 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Mtendee mema jirani yako;
Yohana anaandika katika waraka wake kwamba pendo latoka kwa Mungu mwenyewe maana yeye ndiye aliyetupenda kwanza pale alipotupa wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Yohana katika somo la asubuhi ya leo anaandika kwamba mtu anayesema kwamba anampenda Mungu wakati anamchukia ndugu yake huyo ni muongo! Kwamba unampenda Mungu ambaye humuoni halafu unamchukia ndugu unayemuona? Muongo!
Yohana anatukumbusha kuwapenda ndugu zetu. Hii ni amri toka kwa Mungu kwamba tupendane. Naandika siku zote, kwamba kuhubiri upendo kwa jirani ni rahisi, ila kuuishi ni mtihani. Ni kwa neema ya Mungu tunaweza kupendana kama kundi moja la waaminio katika Ufalme wa Mungu. Mpende jirani yako, umtendee mema. Hii ni amri toka kwa Yesu Kristo. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650