MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 22 JUNI, 2025
SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
TUYASHIKE SANA MAUNGAMO YETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 15/06/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 15/06/2025 ni Washarika 836. Sunday School 86
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Mazoezi ya Kwaya ya Umoja yanaendelea Jumanne ijayo tarehe saa 11.00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya reformation. Wanakwaya walio tayari wanaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati, pia washarika watakaopenda kuimba kwa ajili maandalizi haya ya reformation mnakaribishwa sana.
8. Jumamosi ijayo tarehe 28/06/2025 kutakuwa na tamasha la watoto wa Sunday School litakalofanyika Usharika wa Ukonga K.K.K.T. Wazazi na Walezi mnaombwa siku hiyo kuwaleta watoto hapa kanisani saa 12.30 asubuhi. Sare ya tamasha hilo itakuwa ni Tshirt ambazo zimeandaliwa na Dayosisi. Pia wazazi na walezi mnaombwa kuwaleta watoto ijumaa kwa ajili ya maandalizi yatakayoanza saa 8.00 mpaka saa 9.00 alasiri.
9. Jumapili ijayo tarehe 29/06/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
10. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 29/06/2025 katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi, familia ya Bwana na bibi Jerry Shuma watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kutimiza miaka 20 ya ndoa.
Neno: Zaburi 138 1-3, Wimbo: namba Zawadi Gani Mimi nitamtolea Bwana.
11. Uongozi wa umoja wa Vijana unapenda kuwakaribisha vijana wote kujiunga na timu ya mpira wa miguu kwa ajili ya mashindano ya jimbo, yanayokwenda kwa jina la Kimambo Cup. Pia Kutakuwa na mkesha wa vijana wote siku ya tarehe 4/7/2025 . Vijana wote mnakaribishwa. Aidha Jimbo limeandaa udiakonia tarehe 14-19/7/2025 vijana wote tunakaribishwa kwa ajili ya huduma hiyo.
12. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 12/07/2025
SAA 5.30 ASUBUHI
- Bw. Traviss Tariq Adlam na Bi. Vanessa Nashera Senkoro
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Dr. na Bibi Shuma
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Seppi Mawalla
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin Matandiko
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Harold Kida
14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.