Date:
03-01-2025
Reading:
Maombolezo 3:25-26
Ijumaa asubuhi tarehe 03.01.2025
Maombolezo 3:25-26
[25]BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
[26]Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA na kumngojea kwa utulivu.
Waliomngojea Mwokozi wamuona;
Yeremia baada ya kupitia shida na mateso, akipoteza mali na watoto, anaomboleza akionesha kuwa Upendo wa Mungu huvumilia. Leo asubuhi tunasoma kuwa Bwana ni mwema kwa wote wamtafutao, akiwasihi waungoje wokovu wa Bwana na kumngojea kwa utulivu. Katika kungojea huko, Bwana hutuvumilia, ndio maana hutupa nafasi ya kutubu. Unaitumiaje nafasi hiyo?
Kumngojea kwa utulivu ni kuishi kwa msingi wa neno la Mungu, tukijua wokovu upo kwa ajili yetu. Hatuwezi kuupata huo wokovu bila kutubu dhambi. Tukitubu dhambi tunayo hakika ya wokovu. Amina
Ijumaa njema