Date: 
04-10-2024
Reading: 
Waamuzi 13:2-7

Ijumaa asubuhi tarehe 04.10.2024

Waamuzi 13:2-7

2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.

3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.

4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake;

7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.

Tuwajali watoto wetu katika Bwana;

Somo la asubuhi hii ni mwanzo wa historia ya Samsoni. Mke wake Manoa ambaye alikuja kuwa mama yake Samsoni alitokewa na Malaika akapewa habari njema kuwa atachukua mimba na atazaa mtoto mwanamume. Bila shaka ilikuwa habari njema na ya furaha sana maana mwanamka yule alikuwa tasa. Malaika alimwambia yule mwanamke kwamba mtoto huyo angekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni hata siku ya kufa kwake. 

Ukiendelea kusoma unaona tangazo la kuzaliwa mtoto mwanamume lilipokelewa, na mtoto alizaliwa akaitwa jina lake Samsoni. Leo hatumuongelei Samsoni na yaliyotokea, bali Manoa na mke wake waliomtegemea Mungu akawapa mtoto katika hali ya utasa. Na zaidi, mtoto ambaye alikuwa mnadhiri wa Mungu.

Watoto tulio nao ni zawadi toka kwa Mungu. Hivyo tumshukuru kwa zawadi hii ya watoto, na tuwafundishe kumjua yeye aliye njia ya kweli na uzima. Amina

 

Heri Buberwa