Date: 
01-07-2024
Reading: 
Tito 2:6-8

Jumatatu asubuhi tarehe 01.07.2024

Tito 2:6-8

6 Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;

7 katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,

8 na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

Ninyi ni barua ya Kristo;

Paulo anamwandikia Tito kufundisha yampasayo kila mmoja kwa nafasi yake. Anaandika wazee wafanye nini,vijana, watumwa, na kila awaye yote. Sehemu tuliyosoma ni ujumbe kwa vijana kuwa na kiasi, matendo mema, usahihi na ustahivu. Vijana wanaelekezwa kuishi maisha ambayo neno baya halitadhihirika kwao. 

Ujumbe wa leo ni kwa vijana kama sehemu tu ya familia na Kanisa. Ujumbe huu ni kwa kila mmoja wetu, kwamba tuwe na kiasi, wenye matendo mema, usahihi na ustahivu. Ni muhimu mambo mema kudhihirika kwetu, maana sisi ni barua ya Kristo ambayo watu wanaisoma. Amina

Tunakutakia wiki njema, ukiwa barua ya Kristo 

Heri Buberwa