MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 26 MEI, 2024

SIKU YA UTATU MTAKATIFU

NENO LINALOTUONGOZA

SIKU YA LEO NI

IWENI NA NIA YA KRISTO 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 19/05/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Leo tarehe 26/05/2024 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.  

7.Jumapili ijayo tarehe 02/06/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

8. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwashukuru wazazi na Walezi kwa kuwaandaa watoto kuhudhuria tamasha ambalo limefanyika jana jumamosi tarehe 25/05/2024. Mungu awabariki wazazi na Walezi kwa utayari wenu kwa kuwaruhusu watoto. 

9. Uongozi wa usharika unapenda kuwakumbusha washarika wote walioahidi sadaka za mavuno, na kuchukua vitu vya mnada katika mavuno ya mwaka 2022-2023 kumalizia nadhili zao walizojiwekea mbele za Mungu.

10. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

11. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/06/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 10.00 JIONI KATI YA

  • Bw. Joseph Peter Moshi na Bi. Joyce Joseph Davidson

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 01/06/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Venance Rogasian Mafunga na Bi. Grace Speri Katto

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: kwa Beatrice Lyimo - Undali Street
  • Mjini kati: Kwa Hilda Rwanshane
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Kinondoni: Kwa ……………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………………….
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………..
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Mama Itemba
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa mata

ngazo yetu, Bwana ayabariki