Date: 
27-05-2024
Reading: 
2 Wakorintho 13:14

Jumatatu asubuhi tarehe 27.05.2024

2 Wakorintho 13:14

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Somo la asubuhi hii ni mstari wa mwisho wa Mtume Paulo katika nyaraka alizowaandikia Wakorintho. Ni maneno ambayo tunayatumia mara nyingi wakati wa kuagana panapo kusanyiko katika Kanisa.

Asubuhi ya leo Sala hii ya neema itukumbushe mambo mawili;

Tukae pamoja kwa upendo. Mtume Paulo anatusihi tukae katika ushirika wa Roho Mtakatifu. Ushirika huu unawezekana kwa watu wanaoishi kama ndugu katika Kristo. Ni wito wa Mtume Paulo Kanisa kukaa pamoja katika ibada na maisha yote kwa Utukufu wa Mungu.

Pia, Mtume Paulo anatuonesha kuwa Mungu wetu ni mmoja, katika Utatu Mtakatifu. Kumbe siku zote tumepewa kusali sala hii ili tuzingatie Utatu Mtakatifu. Imani yetu lazima isimame katika Mungu mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina

Uwe na wiki njema. 

 

Heri Buberwa