MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 19 MEI, 2024

SIKU YA KUKUMBUKA KUSHUKA KWA ROHO MTAKATIFU

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

 ROHO MTAKATIFU NGUVU YETU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 12/05/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Jumatatu ijayo yaani kesho tarehe 20/05/2024 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya Pentekoste. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Pili..

7. Jumapili ijayo tarehe 26/05/2024 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.  

8. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/06/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 10.00 JIONI KATI YA

  • Bw. Joseph Peter Moshi na Bi. Joyce Joseph Davidson

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 01/06/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Venance Rogasian Mafunga na Bi. Grace Speri Katto

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

8. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Watatangaziana
  • Mjini kati: Watafanyia hapa usharikani jumamosi saa 1.00 asubuhi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Kinondoni: Kwa ……………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Christopher Kivulenge
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………..
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………..
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

9. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki