Date: 
26-04-2024
Reading: 
Wagalatia 3:1-6

Ijumaa asubuhi tarehe 26.04.2024

Wagalatia 3:1-6

1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?

2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?

3 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?

4 Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli.

5 Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?

6 Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.

Maisha mapya ndani ya Kristo;

Ni maneno makali sana kwa Wagalatia "nani aliyewaroga"? Yesu alihubiriwa kwao kwamba alisulibiwa, akafa na kufufuka, hivyo kuwapa wokovu. Sasa Paulo anahoji kwa nini bado wanashikilia matendo ya sheria? Anawapa mfano, kwamba hata Ibrahimu alihesabiwa haki kwa kumwamini Mungu. 

Mtume Paulo alikuwa anawakumbusha Wagalatia kuwa baada ya Kristo kufa na kufufuka sheria haikuwa na nafasi tena, bali Kristo mwenyewe aliyetukomboa kwa damu yake. Kukumbatia sheria ni kurogwa na kutokuwa na akili, bali kumfuata Kristo kama utimilifu wa sheria ni maisha mapya katika Kristo mwenyewe. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa