Date: 
08-04-2024
Reading: 
Zaburi 104:16-24

Jumatatu asubuhi tarehe 08.04.2024

Zaburi 104:16-24

16 Miti ya Bwana nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

17 Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, Na korongo, misunobari ni nyumba yake.

18 Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari.

19 Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake.

20 Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu.

21 Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu.

22 Jua lachomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao.

23 Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni.

24 Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako.

Tutunze mazingira yetu;

Zaburi hii ya 104 inamsifu Mungu kwa ukuu wake, kwa sababu ya uumbaji wake. Mwandishi anataja uumbaji wa Mungu na uzuri wa dunia aliyoiumba. Ni nchi yenye miti, ndege, milima, wanyama, mwezi, jua, giza, usiku, majira, bahari na vyote viijazavyo dunia. 

Angalia mwandishi anavyompa Mungu Utukufu;

Zaburi 104:31-32

31 Utukufu wa Bwana na udumu milele; Bwana na ayafurahie matendo yake.
32 Aitazama nchi, inatetemeka; Aigusa milima, inatoka moshi.

Katika somo la asubuhi ya leo, mwandishi anatukumbusha kuwa dunia yote hii tunayoishi ni uumbaji wa Mungu. Mungu ametuumba na kutuweka tuifurahie dunia, lakini tuitunze ili iwe sehemu salama ya kuishi sisi na viumbe vyote. Tunapotunza mazingira tunatunza uumbaji wa Mungu. Amina.

Uwe na wiki njema 

Heri Buberwa