Date: 
06-04-2024
Reading: 
Hosea 13:14

Jumamosi asubuhi tarehe 06.04.2024

Hosea 13:14

Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

Tunaitwa kutembea na Yesu mfufuka;

Katika sura ya 13 tunasoma Mungu akiwakumbusha Taifa lake kuwa yeye ndiye Mwokozi wao, ndiye aliyewakomboa kutoka Misri utumwani. Mungu anawapa ujumbe akiwakumbusha jinsi alivyowaongoza jangwani kuelekea nchi ya ahadi;

Hosea 13:4-5

4 Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna Mwokozi.
5 Mimi nalikujua katika jangwa, katika nchi yenye kiu nyingi.

Mstari wa 14 wa somo asubuhi hii ni ahadi ya Mungu kuwakomboa watu wake na kaburi, kuwaokoa na mauti. Ni ahadi ya kuwaokoa watu wote wamwaminio Yesu Kristo kama Mwokozi wao. Kwa njia hii tunaalikwa kutembea na Yesu huyu mfufuka aliye Mwokozi wetu, ili tuweze kuurithi uzima wa milele. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa