Date: 
05-04-2024
Reading: 
Isaya 35:1-2

Ijumaa asubuhi tarehe 05.04.2024

Isaya 35:1-2

1 Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.

2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu.

Tunaitwa kutembea na Yesu mfufuka;

Nabii Isaya alileta ujumbe wa matumaini kwa taifa la Mungu juu ya neema ya Mungu kwao. Anaanza kwa kutumia lugha ya nyika na ukiwa akimaanisha hali isiyokuwa ya kawaida kwa watu wa Mungu. Sasa katika hali hiyo Mungu anaahidi neema. Anaahidi furaha na shangwe, zaidi ipo ahadi ya Utukufu wa Bwana na ukuu wake.

Furaha ya Mungu hukaa kwetu hata sasa. Kufufuka kwa Yesu Kristo ni furaha na shangwe kwetu sisi kama kundi la waaminio, maana ni kwa njia hiyo tumeokolewa. 

Wajibu wetu ni kukaa kwa Kristo mfufuka, ili furaha hii isitupungukie. Furaha isiyoisha katika Bwana ni njia ya kuelekea uzima wa milele. Amina.

Ijumaa njema

Heri Buberwa