Date: 
15-03-2024
Reading: 
Sefania 3:16-17

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 15.03.2024

Sefania 3:16-17

16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa, Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.

17 Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.

Furahini katika Bwana siku zote;

Ujumbe wa unabii ya Sefania ni "Siku ya BWANA" ambayo itatakasa uovu wote katika mataifa yote. Uovu wa Yuda ni kuabudu miungu na kukosa uadilifu. Yuda inatolewa wito wa kutubu;

Sefania 2:3

Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.

Sefania anatoa ujumbe wa wokovu kwa Yuda watiifu na wanyenyekevu (3:12-13)

Mistari tuliyosoma hapo juu kwa sehemu inatoa ujumbe wa wokovu kwa kila atubuye. Ni ahadi ya Mungu kuwa katikati ya watu wamrudiao. Tukiishi maisha ya toba, Kristo hukaa kwetu daima. Amina

Ijumaa njema.

Heri Buberwa