MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 28 JANUARI, 2024

SIKU YA BWANA YA 9 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

WOKOVU WETU NI KWA NEEMA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti.

3.Matoleo ya Tarehe 21/01/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Jumapili ijayo tarehe 04/02/2024 tutamtole Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

6. Kwaya ya Agape inapenda kuwajulisha washarika kuwa wanajiandaa kutembelea watoto wenye vichwa vikubwa na kuwalipia Bima katika Hosptali ya Taifa Muhimbili Moi kama wafanyavyo kila mwaka. Mwaka jana Washarika mliwawezesha kuwalipia watoto 130 kwa kuwalipia bima ya afya na kununua friji kubwa la kuifadhia vyakula maziwa na dawa. Mwaka huu tunatamani kuwalipia angalau watoto 150. Wanaomba washarika muwaunge mkono kwa kutoa fedha, pampas, sabuni, dawa za meno, maji, juice. Unaweza kuwasilisha kwa Mhasibu wa usharika, Parishi Worker au Mtunza hazina wa agape no: 0767214441 Janice kaisi au Acc No. 013874006021 MAENDELEO BANK Jina AGAPE EVANGELICAL SINGER AZANIA FRONT. Washarika walioamua kulipia watoto 10 kila mwaka wanaombwa wawasiliane na uongozi wa Agape kupata taarifa mpya za NHIF. Mungu awabariki sana. 

7. Shukrani – Jumapili ijayo tarehe 04/02/2024 

Ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi

Wagane na Wajane watamshukuru Mungu kwa ulinzi wake mwaka mzima uliopita 2023 na kuwavusha salama mwaka 2024. Baada ya ibada watakuwa na kikombe cha Chai.

Neno: Waebrania 12 : 14, Wimbo: TMW. No. 295

8. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Makwe
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale

9. Ndoa za Washarika.  

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 09/02/2024 

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Shubbi Jesse Mahilane na Bi. Celesta Constantine Speratus

TAREHE 11/02/2024

SAA 8.OO MCHANA

  1. Bw. Dennis Charles Mkony na Bi. Neema Joho Marwa

Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

10. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.