Date: 
17-01-2024
Reading: 
Yohana 2:1-12

Jumatano tarehe 17/12/2024 asubuhi

Yohana 2:1-12

1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.

6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

12 Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko sikusi nyingi.

Mungu hubariki familia zetu

Katika somo la leo tunaona Yesu akifanya muujiza wake wa kwanza akiwasaidia ndugu waliotindikiwa na divai katika harusi yao. Yesu, mama yake na wanafunzi wake walikuwa wameealikwa katika harusi hiyo kama familia. Kwa muujiza huo yesu aliibariki ile familia ile kwenye sherehe yao ya harusi.

Nasi Tunapokuwa na Yesu katika familia zetu, tunabarikiwa pia.

Nawatakia siku njema.

C. Swai.