Date: 
15-11-2023
Reading: 
1 Wathesalonike 1:2-7

Jumatano asubuhi tarehe 15.11.2023

1 Wathesalonike 1:2-7

2 Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.

3 Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.

4 Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;

5 ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.

6 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.

7 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;

Mtume Paulo anawakumbuka watu wa Kanisa la Thesalonike kwa jinsi walivyoshirikiana naye alipowapelekea Injili. Anawakumbuka kwa upendo, akiwasihi kudumu katika Kristo hata ajapo. Anawasisitizia kuishika Injili iliyowafikia kwa njia ya Roho Mtakatifu ili wawe wafuasi wa Kristo daima.

Mtume Paulo anawasihi kumshika Yesu hadi mwisho ili wauone ufalme wake;

1 Wathesalonike 1:8-10

8 Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.
9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;
10 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.

Mstari wa 10 una ujumbe wa kumngojea Kristo mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja. Kumbe tukumbuke kulishika neno la Kristo daima ili kuepuka ghadhabu itakayokuja. Tuvumilie hata mwisho, ili tuurithi uzima wa milele. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa