Date: 
31-10-2023
Reading: 
1Wakorintho 3:11-15

Jumanne asubuhi tarehe 31.10.2023

1 Wakorintho 3:11-15

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.

13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.

Tutengeneze mambo yaliyoharibika;

Mtume Paulo katika sura ya tatu anawaandikia Wakorintho akiwaita watoto wachanga. Anasema anawanywesha maziwa maana chakula hawakiwezi. Paulo anasema walikuwa wachanga kiroho maana bado walikuwa na tabia za mwilini. Waliwatazama viongozi wao badala ya kumtazama Kristo. Paulo anawapa neno la Kristo ambalo ndilo msingi imara wa imani.

Katika somo tulilosoma Paulo anasema hakuna msingi wowote wa Imani tofauti na Yesu Kristo. Mtu ajengaye juu ya msingi ambao ni Kristo nyumba yake huwa imara. Ajengaye kwenye msingi tofauti na Kristo hupata hasara. Paulo anatukumbusha kujenga kwenye msingi imara, yaani kudumu katika imani ya kweli, kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa