Date: 
25-10-2023
Reading: 
Matendo 9:1-9

Jumatano asubuhi tarehe 25.10.2023

Matendo ya Mitume 9:1-9

1 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,

2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.

3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.

4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?

5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.

6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.

7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.

8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.

9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.

Tuheshimu wito tuliopewa na Mungu;

Sauli alikuwa mtu hatari na tishio. Aliwatesa na kuwaua watu wote waliohubiri Injili ya Yesu Kristo. Katika somo la leo asubuhi, tumeona akiwa anaelekea Dameski, ndipo akakutana na Yesu. Hata huko Dameski alikuwa anaenda kuendeleza mateso kwa waaminio. Yesu Kristo aliyekutana naye akamuita kuhubiri, badala ya kuua wanaohubiri. Huyu ndiye Mtume Paulo tunayemsoma leo.

Sauli (Baadaye Paulo) alipokutana na Yesu akaitwa alikuwa mtii. Aliitika wito huo akaanza kuhubiri;

Matendo ya Mitume 9:19-22

19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?
22 Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.

Sauli aliheshimu wito aliopewa na Kristo.

Nasi tunaalikwa kuheshimu wito wetu, tumwamini na kumtumikia Mungu daima. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa