Date: 
07-10-2023
Reading: 
Isaya 54:12-13

Jumamosi asubuhi tarehe 07.10.2023

Isaya 54:12-13

12 Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.

13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

Tuwalee watoto katika njia ya Bwana;

Somo la asubuhi ya leo ni sehemu ya ujumbe wa Bwana kwa taifa la Israeli mara baada ya kuwa wametoka uhamishoni Babeli. Bwana anawapa uhakika wa kuishi akiwalinda katika maisha yao. Jamii nzima inapewa uhakika wa kutunzwa na Bwana, watoto kufundishwa na Bwana, na amani kutawala katikati yao.

Baada ya shida nyingi uhamishoni na kurejea, Bwana anatoa tumaini lake kwa watu wake. Bwana hakuishia hapo, alimtuma Yesu Kristo afe na kufufuka ili kuukomboa Ulimwengu. Mpango wa Mungu siku zote ni amani yake kukaa katikati ya watu wake, wadumu katika wokovu. Mwamini Yesu uokolewe. Amina.

Jumamosi njema

Heri Buberwa