Date: 
04-10-2023
Reading: 
Waefeso 6:1-4

Jumatano asubuhi tarehe 04.10.2023

Waefeso 6:1-4

1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.

4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

Tuwalee watoto katika njia ya Bwana;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Efeso juu ya uwajibikaji katika familia. Anawaambia watoto kuwatii wazazi wao, ili wapate siku nyingi na heri duniani. Hapa Mtume Paulo anawakumbusha amri iliyokuwepo tokea zamani;

Kutoka 20:12

Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Mstari wa nne unawaelekeza wazazi kutimiza wajibu wao katika kuwalea watoto. Mstari unasema tuwafundishe adabu na maonyo ya Bwana. Kumbe wazazi tunao wajibu wa kuwafundisha watoto adabu na utii kwa wazazi ili wapate heri duniani. Mafundisho yetu kwa watoto yalenge wao kukua katika ushuhuda kwa Kikristo. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa