Date: 
03-10-2023
Reading: 
Luka 18:15-17

Jumanne asubuhi tarehe 03.10.2023

Luka 18:15-17

15 Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse; lakini wanafunzi walipoona waliwakemea.

16 Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao.

17 Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.

Tuwalee watoto katika njia ya Bwana;

Wanafunzi wa Yesu hawakufurahishwa na kitendo cha watu kuwaleta watoto wao kwa Yesu. Hawakuwa tayari watoto wamkaribie Yesu. Kumbe mawazo yao yalikuwa tofauti kabisa na yale ya Yesu. Wakati wao wanazuia watoto kuletwa kwa Yesu, Yesu anasema waache waje kwangu. Tena Yesu anakazia kuwa asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto hauingii kamwe. 

Yesu anatufundisha kuwaleta watoto kwake, yaani tuwalee watoto katika njia sahihi katika kumfuata Kristo. Tuwape watoto elimu na mahitaji mengine yote muhimu, lakini tuwape neno la Mungu kama msingi wa maisha yao. Kwa kuwaleta watoto kwa Yesu, tunaandaa kizazi bora kuanzia familia, Kanisa na Taifa kwa ujumla. Amina.

Jumanne njema.

Heri Buberwa