Date: 
30-09-2023
Reading: 
Kutoka 34:5-9

Jumamosi asubuhi 30.09.2023

Kutoka 34:5-9

5 Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana.

6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

8 Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu.

9 Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.

Mungu amejaa huruma;

Musa anamtangaza Bwana kama mwenye wingi wa huruma, fadhili, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema na kweli. Yeye husamehe uovu na dhambi zote. Mstari wa 7 unaonesha kuwa Mungu hamhesabii mwovu kuwa hana hatia, huwapatiliza vizazi na vizazi kwa dhambi za baba zao. Lakini baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, atubuye dhambi zake husamehewa, na ndiyo maana alisema;

Mathayo 11:28

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Musa alikuwa anatoa tangazo kwa wana wa Israeli juu ya huruma za Bwana. Tangazo hili linadumu kwetu hala leo, kwamba Mungu amejaa huruma, ni mwenye haki, fadhili, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema na kweli. Tukimfuata Yesu mwenye huruma tutaurithi uzima wa milele, Amina.

Heri Buberwa 

Mlutheri