Event Date: 
17-09-2023

Jumapili ya tarehe 17 Septemba 2023, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, Chaplain Charles Mzinga aliongoza ujumbe wa Usharika kwenye ziara iliyofanyika mtaa wa Tabora, miongoni mwa mitaa inayotunzwa na Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral.

Akiwa mtaani hapo, Chaplain Mzinga aliongoza ibada takatifu iliyohudhuriwa na washarika wa mtaa huo. Katika ibada hiyo, jumla ya watoto wadogo saba (7) walibatizwa na washarika walipata fursa ya kushiriki Meza ya Bwana.

Pia ibada hiyo iliambatana na mavuno yaliyotolewa na washarika wa mtaa huo na kupokelewa na Chaplain Mzinga.

Baada ya Ibada hiyo Chaplain Mzinga na ujumbe wake walitembelea na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika mtaa huo.

Baadhi ya matukio tofauti tofauti katika picha kutoka kwenye ziara hiyo; 

Ripoti hii imeandaliwa na; Cuthbert Swai