MATANGAZO YA USHARIKA 

 LEO TAREHE 03 SEPTEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA 13 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA  NI

JIRANI WETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 27/08/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Jumapili ijayo tarehe 10/09/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae. Aidha siku hiyo itakuwa ni ubatizo wa Watoto wadogo na kurudi kundini. Watakao hitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji. 

6. Umoja wa Wanawake Azania Front unawatangazia Wanawake wote semina itakayofanyika katika kituo chetu cha Kiroho Kiharaka jumamosi ijayo tarehe 9 Septemba 2023 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni. Usafiri wa kuelekea Kiharaka utakuwepo hapa kanisani saa 12 kamili asubuhi. Ili kuweza kufanya maandalizi na usafiri, tunaomba Wanawake wajiandikishe kupitia WhatsApp Group ya UWA au ofisini kwa Parish Worker.

7. Kwaya Uinjilisti Agape leo Watafanya uzinduzi wa Audio Flash ya nyimbo katika Ibada zote Lengo ni kueneza Injili isambae na kusaidia kwaya kwenye Safari ya Uinjilisti Mwanza wiki ijayo Pamoja na Kusaidia Maandalizi ya Video zijazo. Washarika tunaombwa mnaombwa kuwaunga mkono. 

8. SHUKRANI - JUMAPILI IJAYO TAREHE 10/09/2023 

Katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi

  • Mama Omega Mongi atamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyomtendea ikiwa ni Pamoja na kufikisha miaka 75 ya kuzaliwa.

Neno:Zaburi 124, WimboTMW 428, na Kwaya ya Wanawake

9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 23/09/2023 

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE USHARIKA WA NYABWEGIRA 

SAA 4.00 ASUBUHI

  • Bw. Mwema Tikansimile na Bi. Happyness Jonhnson 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Seppi Mawala
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw & Bi Kenneth Zebedayo
  • Kinondoni: Kwa PROFESA G. MMARI
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: BW & BI MCHARO MLAKI
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bw & Bi. Robinson Monyo

11. Zamu: Zamu za wazeeni ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.