Date: 
29-08-2023
Reading: 
Mithali 26:27-28

Jumanne asubuhi tarehe 29.08.2023

Mithali 26:27-28

27 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

28 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

Matumizi ya Ulimi;

Ipo tabia ya baadhi yetu kuwatakia wengine mabaya, jambo ambalo ni kinyume na Imani yetu. Katika somo la asubuhi hii, mwandishi anatumia dhana ya kuchimba shimo na kutumbukia mwenyewe, kubiringisha jiwe likakurudia. Anataka watu wawaze na kutenda mema, na mema hayo yawajie wenyewe.

Somo linazuia kutumia ulimi kusema uongo, maana huleta chuki. Lakini mwandishi anazuia kujipendekeza pia. Kujipendekeza kunaweza kusababisha kuumiza wengine, maana anayejipendekeza hutafuta kupendwa. Tunaelekezwa kuishi tukipendana na kuhurumiana katika Bwana. Amina

Heri Buberwa