Date: 
28-08-2023
Reading: 
Yakobo 5:12

Jumatatu asubuhi tarehe 28.08.2023

Yakobo 5:12

Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.

Matumizi ya Ulimi;

Kuapa lilikuwa jambo la kawaida sana kwa Wayahudi. Inaonekana ilikuwa dhahiri hadi Yakobo akakemea jambo hili, akiwaambia wasiape kwa mbingu na nchi, bali wasimame katika kweli ya neno la Mungu. 

Yakobo anakumbusha fundisho la Yesu kwenye hotuba ya mlimani;

Mathayo 5:34-37

34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Yakobo anazuia viapo vya mazungumzo kila wakati. Anasisitiza kusimama katika kweli ya Mungu. Hamaanishi kutoapa katika kazi zetu za ofisi, bali katika mazingira hayo, kweli yetu iwe kweli, na siyo iwe siyo. Yakobo anamaanisha kwamba tutende yote katika Kristo, na siyo kwa akili zetu.

Ndiyo na siyo zetu zinasikika kwa njia ya ulimi. Uwasilishaji wetu kwa njia ya ulimi uwe wenye Utukufu kwa Mungu. Amina.

Uwe na wiki njema yenye matumizi mazuri ya Ulimi.

 

Heri Buberwa