Date: 
11-08-2023
Reading: 
Methali 3:21-26

Ijumaa asubuhi tarehe 11.08.2023

Mithali 3:21-26

21 Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara.

22 Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako.

23 Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa.

24 Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.

25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.

26 Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.

Tuenende kwa hekima;

Baada ya Suleimani kufundisha juu ya kumcha Bwana kama chanzo cha maarifa, kujua hekima na adabu katika sura ya kwanza, sura ya pili na ya tatu tunayosoma asubuhi hii inafundisha juu ya kulishika neno la Mungu. Katika somo tulilosoma tunaona kuwa kushika neno la Mungu humpeleka aaminiye katika njia salama. Neno la Mungu humfanya mtu asiwe na hofu, tumaini likiwa kwa Bwana.

Suleimani anatukumbusha kulishika neno la Mungu katika Mithali tulizosoma. Tunapomsoma Suleimani, tulishike neno la Mungu kwa kumtazama Kristo aliye neno toka mbinguni. Tusichoke kumuomba Yesu Kristo atujalie hekima itokayo kwake, ili tutende kadri ya mapenzi yake. Amina.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa