MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 06 AGOSTI, 2023
SIKU YA BWANA YA 9 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUENENDE KWA HEKIMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 30/07/2023
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
5. Leo 06/08/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.
6. Jumapili ijayo tarehe 13/08/2023 ni siku ya ubatizo wa Watoto Pamoja na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
7. Kwaya Ya Upendo inakodisha Bus lao kwa matumizi ya biashara, wanaomba Washarika, Vikundi vyetu hapa Usharikani mnapo hitaji usafiri wa Bus tafadhali karibuni mtumie Bus letu, Wanawahakikishia Kupata huduma nzuri. Karibuni Sana. KWA MAWASILIANO WASILIANA NA MAKAMU MWENYEKITI WETU DADA LINDA FELISHIAN +255655884657. Mungu akubariki sana
8. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 13/08/2023
IBADA YA KWANZA SAA 4.30 ASUBUHI
- Bibi Naiz Mavura na Watoto wake watamshukuru Mungu shukrani kwa ajili ya mambo mema mengi aliyowatendea ikiwa pamoja na kijana wake Nassa kufaulu High School na kupata nafasi ya kujiunga na University, Bibi Naiz kupanda cheo, Kijana wake mdogo kutimiza miaka 14 tarehe 13 mwezi Agosti na kupata faraja tangu mume wake mpenzi alipotwaliwa miaka 7.
Neno: Zaburi 23, Wimbo: Anibariki nami nitaimba(Kwaya Kuu)
9. Tarehe 30.09.2023 na Tarehe 01.10.2023 itakuwa ni Sikukuu ya Mikaeli na watoto. Hivyo tarehe 30.09.2023 watoto watavaa tshirt ambazo zinauzwa kwa bei ya 13,000 na zinapatikana ofisini kwa Parish Worker. Tarehe 01.10.2023 watavaa vitenge vya kiharaka.
10. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 19/08/2023
NDOA HII ITAFUNGWA PAROKIA YA MTAKATIFU IMMACULATA UPANGA KATI YA
SAA 7.00 MCHANA
- Bw. John-Paul Andrew Chenge na Bi. Allegra Victor Kida
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 12/08/2023
NDOA HII ITAFUNGWA KKKT KANISA KUU MJINI KATI ARUSHA KATI YA
- Bw. Isaya Zakaria Mollel na Bi. Klemmie Imwaga Majamba
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Whitsun Moshi.
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:Kwa Mama Mamkwe
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Bwana na Bibi Rweikiza
- Kinondoni: Kwa Profesa G. Mmari
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Buchanagandi
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Dr. Mbowe
12. Zamu: Zamu za wazeeni ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.