Date: 
07-08-2023
Reading: 
Methali 9:1-9

Jumatatu asubuhi tarehe 07.08.2023

Mithali 9:1-9

1 Hekima umeijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba;

2 Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia.

3 Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana,

4 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,

5 Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya.

6 Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.

7 Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.

8 Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.

9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;

Tuenende kwa hekima;

Asubuhi hii tunaelekezwa kutafakari juu ya kuenenda kwa hekima. Sura ya 9 inaalika waamini kuiomba hekima ya Mungu. Mstari wa 6 unakazia kuacha ujinga na kwenda katika njia ya ufahamu. Tunazidi kuona kuwa mwenye hekima akikaripiwa, humpenda aliyemkaripia. Kwa muktadha huu, hekima inaonekana kuwa kiwango cha juu cha maarifa katika Bwana katika kuamua na kutenda kwa usahihi.

Suleimani aliona kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, na katika kumcha Bwana huko aliwaasa watu kuenenda kwa hekima. Ukisoma mbele kidogo Suleimani anasema kwamba;

Mithali 9:10

Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

Neema ya Mungu iwe nasi, tuenende na kutenda yote kwa hekima itokayo mbinguni.

Uwe na wiki njema yenye hekima.

 

Heri Buberwa