Date: 
03-08-2023
Reading: 
Yoshua 7:6-13

Alhamisi asubuhi tarehe 03.08.2023

Yoshua 7:6-13

6 Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.

7 Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng'ambo ya Yordani

8 Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao?

9 Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?

10 Bwana akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?

11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.

12 Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.

13 Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.

Wema wa Mungu watuvuta tupate kutubu;

Israeli walitenda dhambi kwa kila kitu kilichowekwa wakfu kama mstari wa kwanza unavyosomeka;

Yoshua 7:1

Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli.

Wakati huu Yoshua ndiye alikuwa kiongozi wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Akawatuma watu kupeleleza mji waliokuwa wanauendea, wakapigwa sana.

Ndipo tunamsoma Yoshua akirarua mavazi yake na kumlilia Bwana, maana aliona walikuwa wanaelekea kuangamia.

Mstari wa 13 unaonesha Mungu akimwinua Yoshua na kumwambia awatakase watu, na kuwahakikishia kuwa kila kilichowekwa wakfu kiko katikati yao. Pamoja na kumkosea Mungu, bado Israeli walitakaswa. Nasi tunapokosa, Yesu yuko tayari kutusamehe. Wajibu wetu ni kutubu. Amina.

Uwe na siku njema.

Heri Buberwa