MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 30 JULY, 2023

SIKU YA BWANA YA 8 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI 

WEMA WA MUNGU WATUVUTA TUPATE KUTUBU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 23/07/2023   

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Leo tarehe 30/07/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.

6. Jumapili ijayo tarehe 06/08/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

7. Kwaya Ya Upendo inakodisha Bus lao kwa matumizi ya biashara, wanaomba Washarika, Vikundi vyetu hapa Usharikani mnapo hitaji usafiri wa Bus tafadhali karibuni mtumie Bus letu, Wanawahakikishia Kupata huduma nzuri. Karibuni Sana. KWA MAWASILIANO WASILIANA NA MAKAMU MWENYEKITI WETU DADA LINDA FELISHIAN +255655884657. Mungu akubariki sana 

8. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwaalika vijana wote kujiunga na kikundi cha maigizo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mashindano,siku za zoezi ni Jumatatu saa kumi na moja jioni na Jumamosi saa kumi jioni.Mungu awabariki.

9. Mazoezi ya Mikaeli na Watoto kwa lugha ya kingereza yanaendelea kila siku ya jumamosi kuanzia saa 3.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchanga. Wazazi mnaombwa kuwaleta Watoto kwa wakati uliopangwa. Mungu awabariki.

10. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 06/08/2023

IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Naomi Kaale Ohowa pamoja na familia anapenda wanapenda kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowajalia ikiwemo zawadi ya mtoto. 

Neno:Isaya 12:4-5, Wimbo: Heri kumjua Yesu Bwana Na. 175

  • Onesmo Abrahamu atamshukuru Mungu kwa kumfikisha salama miaka 35 ya Kuzaliwa siku ya 31/07/2023 na 35 ya Ubatizo kanisani Azania Front Cathedral, Kumfanikisha Kutimiza ahadi aliyoahidi katika Fomu ya ahadi ya Kujiunga na kwaya ya Uinjilisti AGAPE, Kumpitisha Salama katika Majaribu na shida za Kiafya na Kiuchumi na zingine mbalimbali maishani.

Neno: Yoshua 1:8, Wimbo: Nasubiri kwa hamu(Kwaya ya Agape)

11. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 19/08/2023

NDOA HII ITAFUNGWA PAROKIA YA MTAKATIFU IMMACULATA UPANGA KATI YA

SAA 7.00 MCHANA

  • Bw. Paul Andrew Chenge na Bi. Allegra Victor Kida

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 12/08/2023

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT KANISA KUU MJINI KATI ARUSHA KATI YA

  • Bw. Isaya Zakaria Mollel na Bi. Klemmie Imwaga Majamba

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

12.. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Towo
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Bw & Bi James Monyo 
  • Kinondoni: Kwa Prof. & Bibi Kulaba
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. & Bibi David Ruhago
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Profesa William Matuja

13. MAHUDHURIO YA IBADA ZA JUMAPILI ILIYOPITA.

WATU WAZIMA - 553

14. Zamu: Zamu za wazee ni ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.