MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 JULY, 2023

SIKU YA BWANA YA 7 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

UCHAGUZI WA BUSARA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 16/07/2023   

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Huduma ya Mana imeandaa Kongamano la Kitaifa la Maombi la 15, litakaloanza tarehe 08 hadi 11/08/2023, University of Dodoma, Dodoma. Kufika ni tarehe 07/08/2023 kwa ajili ya kuhakiki usajili ili uruhusiwe kuingia ukumbi wa maombi. Ada ya usajili ni Tsh. 100,000/= kwa mtu mmoja; kwa ajili ya malazi, chai ya asubuhi, chakula cha mchana na jioni. Nauli haimo kwenye hesabu hii. Mwisho wa usajili ni kesho tarehe 24/07/2023. Fomu za kujiandikisha zinapatikana Ofisi ya huduma ya Mana iliyoko Luther House ghorofa ya tatu (3).

6. Jumapili ijayo tarehe 30/07/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

7. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 30/07/2023 FAMILIA MBILI ZITAMSHUKURU MUNGU

IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI.

  • Mzee Timon Msangi na familia yake watamshukuru Mungu kwa Mzee Msangi Kufikisha miaka 84 tarehe 24.07.2023. Pamoja na mambo mengi aliyowatendea. 

Neno: Zaburi 71:6-12. Wimbo: TMW 295 (Mungu amenihurumia )

IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI.

  • Familia ya Bwana na Bibi Mcharo Mlaki watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea.

Neno: 1 Yoh 4:7-8, Wimbo: 295 (Mungu amenihurumia)  

8. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kutoa shukrani zao kwa vijana wote, pamoja na washarika walioshiriki katika ibada ya sikukuu ya vijana. Pia wanaomba vijana wote ambao hawakujaza form ya kujiunga na umoja wa vijana, bado fomu zipo wawaone viongozi wa vijana. Mungu awabariki sana.

9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 12/08/2023

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT KANISA KUU MJINI KATI ARUSHA KATI YA

  • Bw. Isaya Zakaria Mollel na Bi. Klemmie Imwaga Majamba

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 29/07/2023

NDOA HII ITAFUNGWA PAROKIA YA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY KATI YA

  • Bw. Frank Martin Mollel na Bi. Miriam Alex Malasusa

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Kimweri
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:Kwa Mama Mamkwe
  • Mjini kati: itafanyika hapa Usharikani jumamosi saa 1.00 asubuhi
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Bw & Bi James Monyo 
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
  • Upanga: Kwa Suzan Mboya

11. MAHUDHURIO YA IBADA ZA JUMAPILI ILIYOPITA.

WATU WAZIMA - 667

12. Zamu: Zamu za wazeeni ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki

.