Date: 
18-07-2023
Reading: 
Mwanzo 2:12-23

Jumanne asubuhi tarehe 18.07.2023

Mwanzo 2:18-23

18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.

20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.

21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Amri ya upendo;

Tunasoma juu ya uumbaji wa Mungu. Mungu anampa Adamu usingizi mzito na anatwaa ubavu mmoja toka kwake. Baada ya kutwaa ubavu ule Mungu anaufanya kuwa mwanamke. Adamu naye anampokea mwanamke huyo kwa shukrani.

Tunachosoma leo asubuhi ni uumbaji wa mwanamke. Mungu alipoanza kumuumba mwanamke alisema "si vema huyo mtu awe peke yake...."

Hii ni ishara ya upendo, kwamba Adamu asikae peke yake. Mungu alimpenda Adamu akampa Hawa. Kwa upendo huo huo alimtuma Yesu atuokoe. Leo anatuamuru kupendana. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa