Date: 
15-07-2023
Reading: 
Yeremia 1:17-19

Jumamosi asubuhi tarehe 15.07.2023

Yeremia 1:17-19

17 Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao.

18 Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.

19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.

Mtu akinitumikia na anifuate;

Nabii Yeremia alipoitwa na Bwana kuwa Nabii wake alisema asingeweza kusema na watu maana alikuwa mtoto. Bwana alimwambia yeye ndiye alikuwa amemuita, na angemwezesha kupeleka ujumbe wake. Asubuhi hii tumesoma Bwana akimuamuru Yeremia kuondoka kupeleka neno lake. Anamhakikishia kuwa atampigania katika unabii wake, atashinda.

Katika somo tulilosoma, Bwana alikuwa anapeleka ujumbe wake kwa Taifa lake kupitia kwa Nabii Yeremia aliyemuita. Bwana aliwatuma manabii wengi, na baadaye alimtuma Yesu Kristo kutuletea wokovu kwa njia ya kifo msalabani. Tunaalikwa kudumu katika neema hii ya wokovu aliouleta Yesu tukimtumikia na kumfuata. Amina.

Jumamosi njema.

Heri Buberwa