Date: 
14-07-2023
Reading: 
Marko 1:19-20

Ijumaa asubuhi tarehe 14.07.2023

Marko 1:19-20

19 Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao.

20 Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata.

Mtu akinitumikia na anifuate;

Yesu alikaa jangwani kwa siku arobaini akijaribiwa na Ibilisi, na kwa neno la Mungu alishinda majaribu. Baadaye akabatizwa na Yohana, tayari kwa kazi yake ambapo asubuhi hii tunaona akiwaita Yakobo wa Zebedayo, Yohana nduguye ambao walikuwa wavuvi. Yakobo na Yohana walimuacha baba yao wakamfuata Yesu, na huo ulikuwa mwanzo wao kumfuata Yesu.

Mistari hii ya Injili ya Marko inatukumbusha ujio wa Yesu hapa duniani. Aliwaita Yakobo na Yohana akiwaambia wamfuate, nao atawafanya kuwa wavuvi wa watu. Tayari alikuwa amewaita kumfuata na kumtumikia.

Wito huu wa Yesu unadumu hata sasa, ambapo Yesu anatuita kumwamini na kumtumikia sasa na hata milele. Amina.

 

Heri Buberwa