Date: 
29-06-2023
Reading: 
Ezra 9:5-9

Alhamisi asubuhi tarehe 29.06.2023

Ezra 9:5-9

5 Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu;

6 nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni.

7 Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.

8 Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.

9 Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, kuisimamisha nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu.

Neema ya Mungu yatuwezesha;

Baada ya Taifa la Mungu kutambua dhambi yao, walitetemeka kwa neno lililotoka kwa Mungu wa Israeli. Sasa kinachoonekana asubuhi hii ni ibada iliyofuatia ikiambatana na sadaka. Walimshukuru Mungu kwa kuwa nao siku zote, wakatubu dhambi zao na kutoa sadaka. Katika mstari wa 9 wanakiri kuwa watumwa, ambao Mungu hakuwaacha.

Tunapolisikia neno la Mungu tunawajibika kulisikia na kulishika, maana Mungu hutujia kwa njia ya neno lake. 

Tuendele kuhudhuria ibada, tumwadudu Bwana na kumtolea sadaka, maana yeye ndiye aliye nasi siku zote. Amina.

Heri Buberwa