Date: 
24-06-2023
Reading: 
Isaya 49:14-21

Jumamosi asubuhi tarehe 24.06.2023

Isaya 49:14-21

14 Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.

15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

17 Watoto wako wafanya haraka, hao wakuharibuo, nao waliokufanya ukiwa, watatoka kwako.

18 Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema Bwana, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi.

19 Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali.

20 Watoto ulionyang'anywa watasema masikioni mwako, Mahali hapa ni pembamba, hapanitoshi; nipe nafasi nipate kukaa.

21 Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami ni peke yangu, nimehamishwa, ninatanga-tanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, naliachwa peke yangu; hawa je! Walikuwa wapi?

Mungu hutunza Kanisa lake;

Nabii Isaya anaandika juu ya Mungu kutunza watu wake. Anatoa mfano wa jinsi mwanamke asivyoweza kumsahau mtoto wake anayenyonya, akisema upendo wa Mungu ni zaidi ya hapo. Katikati ya kundi linalosema Mungu ameniacha, Isaya anasema Mungu amewaweka watu wake kwenye kiganja cha mkono wake.

Ujumbe wa Isaya ni kwamba Mungu yuko na watu wake daima. Hii ilikuwa wakati wa Agano la kale. Lakini tokea wakati huo Mungu hakuacha kuwa na watu wake, ndiyo maana alimtuma Yesu kuukomboa Ulimwengu.

Upendo wake wadumu milele.

Karibu kwa Yesu.

Jumamosi njema 

 

Heri Buberwa