MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 18 JUNI, 2023

NENO LINALOTUONGOZA NI

MUNGU HUTUNZA KANISA LAKE 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 11/06/2023

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.  

6. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia Washarika wenye Watoto wa Kipaimara mwaka wa pili kuwa kutakuwa na mtihani ngazi ya kwanza ya Dayosisi tarehe 25/06/2023 ambao utaanza saba na nusu. Hivyo wazazi mnaombwa kusaidia kuwahimiza Watoto kufika mapema na kufanya mtihani huo.

7. Uongozi wa Jimbo utahitimisha kambi ya Watoto Kijimbo siku ya jumanne tarehe 20/06/2023 katika Usharika wa Kitunda Relini. Hivyo kila Usharika umepangiwa Kwenda Watoto 30 tu. Wale wazazi ambao Watoto wao wamechaguliwa mnaombwa Watoto wafike hapa Kanisani saa moja wakiwa wamekunywa chai ili kuanza safari ya kuelekea Kitunda. Mungu awabariki

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 24/06/2023

SAA 10.00 JIONI

  • Bw. Albert Ernest Swai na Bi. Grace John Msangi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  •  Oysterbay na Masaki: Kwa Capt. na Bibi Mkonyi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Mjini kati: Watafanyia hapa Usharikani jumamosi saa 1.00 asubuhi 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
  •  
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha
  • Tabata: Kwa Mchungaji Kibona

10. MAHUDHURIO YA IBADA JUMAPILI ILIYOPITA TAREHE 11/06/2023

- WATU WAZIMA 815

- SUNDAY SCHOOL 238

11. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.