Date: 
09-06-2023
Reading: 
1Yohana 4:1-3

Ijumaa asubuhi 09.06.2023

1 Yohana 4:1-3

1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.

3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.

Mungu mmoja; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Yohana katika sura hii ya nne anaongelea kuzitafakari roho kama zote zinatoka kwa Bwana, maana kuna manabii wengi wa uongo wanaotokea kwa njia ya kujifanya wana Roho wa Mungu. Yohana analiita Kanisa kumjua Roho wa Mungu, pale Kristo anapohubiriwa katika kweli yake. 

Ujumbe huu unatutaka kuishi kwa kumfuata Yesu katika kweli yake tukiepuka mafundisho ya uongo. Mafundisho ya uongo tunayaepuka kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ambaye hutuwezesha kutambua roho zisizofaa. Mungu atusaidie kuzitambua roho zinazoweza kutupoteza ili tusimuache. Amina 

Siku njema.

Heri Buberwa