Date: 
07-06-2023
Reading: 
Luka 3:21-22

Jumatano asubuhi tarehe 07.06.2023

Luka 3:21-22

21 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Yesu anabatizwa, na baada ya kubatizwa mbingu zinafunguka. Roho Mtakatifu anamshukia na sauti inatoka mbinguni kwa Baba ikimtambulisha kama Mwana mpendwa. Ubatizo ulikuwa muhimu kwake, tayari kuianza kazi yake.

Tunauona Utatu Mtakatifu katika ubatizo wa Yesu.

-Sauti inayomtambulisha Yesu inatoka mbinguni kwa Baba 

-Yesu ndiye anabatizwa

-Roho Mtakatifu anamshukia Yesu baada ya kubatizwa.

Kumbe Mungu yupo katika Utatu Mtakatifu. Nasi tuyatende yote kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa