Date: 
06-06-2023
Reading: 
Warumi 16:25-27

Jumanne asubuhi tarehe 06.06.2023

Warumi 16:25-27

25 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,

26 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.

27 Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Mtume Paulo anahitimisha barua yake kwa Warumi kwa kumtukuza Mungu awezaye kuwafanya watu wake imara sawasawa na neno lake. Paulo anaonesha kuwa Mungu huwafanya watu wake imara tangu kale, na milele yote. Na kwa sababu hiyo, anampa Utukufu milele yote.

Tunachokiona Paulo anapohitimisha waraka wake kwa warumi ni kuwa Mungu aliyewaumba watu wake, huwalinda, huwatunza na kuwabariki milele yote. Wajibu wa kila aaminiye ni kulishika neno lake ili Mungu asimuache. 

Tunaalikwa kulishika neno la Mungu ili Mungu atufanye imara siku zote za maisha yetu, hata uzima wa milele. Amina.

Jumanne njema.

 

Heri Buberwa