Date: 
17-05-2023
Reading: 
Yakobo 1:5-7

Hii ni Pasaka 

Jumatano asubuhi tarehe 17.05.2023

Yakobo 1:5-7

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

Ombeni katika jina la Yesu;

Yakobo anaandika juu ya aonaye kupungukiwa na hekima kuomba kwa Mungu. Hekima humuongoza aaminiye kuwaza, kunena na kutenda kwa usahihi. Kumbuka tunamkosea Mungu kwa kuwaza, kunena na kutenda. Yakobo kwa kulitambua hili, analielekeza Kanisa kuomba hekima ya Mungu ili kuishinda dhambi.

Yakobo anatukumbusha kuishi tukiomba, maana pasipo kuomba hatuwezi kuwa na hekima ya kuenenda kwa usahihi. Mkazo wa Yakobo ni kuomba kwa Imani. Imani ya kweli hutufanya kumwendea Mungu itupasavyo hivyo kutupa haja zetu. Tudumu katika sala kwa imani ili maisha yetu yawe yenye ushuhuda. Amina.

Jumatano njema.

 

Heri Buberwa