Date: 
15-05-2023
Reading: 
Mithali 30:7-9

Hii ni Pasaka 

Jumatatu asubuhi tarehe 15.05.2023

Mithali 30:7-9

7 Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa.

8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.

9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.

Ombeni katika jina la Yesu;

Bwana Asifiwe;

Tunasoma ujumbe ambao ni wa kumtegemea Bwana kwa njia ya Sala. Tunaisoma sala inayomuomba Bwana kuondoa ubatili na uongo. Lakini pia lipo ombi la haki toka kwa Bwana, yaani sala ya kupewa mahitaji muhimu kama inavyostahili. Sala inaomba kutoridhika na mambo ya dunia na kumsahau Bwana, bali neema ya Mungu kuwa juu ya aaminiye ili asimsahau Mungu wake.

Muktadha wa ujumbe tuliousoma ni kuishi kwa kumtegemea Bwana, kwa njia ya Sala. Tunaona kwamba tunatakiwa kuishi kwa njia ya sala, lakini tukimuomba Bwana. Tumwendee Bwana kwa unyenyekevu, tukiomba awe nasi katika maisha yetu ya kila siku. Tukumbuke kuishi kwa kuomba, na kuomba kwa jina la Yesu.

Uwe na wiki njema.

Heri Buberwa