Date: 
23-03-2022
Reading: 
Mwanzo 2:4b-15

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 23.03.2022

Mwanzo 2:4b-15

4b. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.

11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;

12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.

13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.

14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

Tutunze uumbaji;

Tunasoma Mungu akiumba dunia, lakini akiumba mwanadamu (7). Baadaye Mungu anapanda bustani na kumweka huyo mtu. Mstari wa 15 tunasoma Mungu akimuweka mwanadamu kwenye bustani ailime na kuitunza.

Jumatano ya leo tunaona kuwa Mungu alimuweka mwanadamu duniani, ili mwanadamu aitunze hiyo dunia, yaani uumbaji wake. Tunautimiza wajibu huu? Hili ni agizo la Bwana, hivyo tunawajibika kulitii, yaani tuitunze dunia tuliyopewa kuishi na Bwana.

Uwe na siku njema.