Date: 
05-06-2021
Reading: 
Mwanzo 1:1-5 (Genesis 1:1-5)

JUMAMOSI TAREHE 5 JUNI 2021, MORNING

Mwanzo 1:1-5

1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Asubuhi hii tunaisoma historia ya uumbaji, mwanzoni kabisa. Tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi. Tunaona pia Roho wa Mungu akitulia juu ya vilindi vya maji.

Huu ni uthibitisho wa Mungu muumbaji. Alianza kuumba dunia, akamuumba mwanadamu, na vingine vyote. Mungu alitutengenezea sehemu nzuri ya kuishi, yaani dunia tuliyomo. Ameipa uzuri dunia ili tuifurahie.

Uumbaji wa Mungu ni alama ya Upendo kwetu. Ndio maana baada ya uumbaji, hakutuacha, akamtuma Yesu Kristo kufa msalabani, lakini pia akatupa Roho Mtakatifu kwa utakaso. Hivyo asili ya Mungu ni upendo.

Tunafanya nini kwa Mungu wetu aliyetuumba, na kutuletea wokovu? Tumwamini, tumpokee, tumfuate, na kumtii ili mwisho wetu uwe mwema.

Asubuhi njema.


SATURDAY 5TH JUNE 2021, MORNING

Genesis 1:1-5 [NIV]

1 In the beginning God created the heavens and the earth. Now the earth was formless and empty, darkness was over the surface of the deep, and the Spirit of God was hovering over the waters.

And God said, “Let there be light,” and there was light. God saw that the light was good, and he separated the light from the darkness. God called the light “day,” and the darkness he called “night.” And there was evening, and there was morning—the first day.

Read full chapter

One God;

Father, Son and Holy Spirit;

This morning we read the history of creation, at the very beginning. We see God creating the heavens and the earth. We also see the Spirit of God resting on the depths of the waters.

This is the proof of God the creator. He began to create the world, created man, and everything else. God made the best place for us to live — the earth. He has given the world beauty so that we can enjoy it.

God's creation is a symbol of Love for us. That is why after creation, He did not leave us, He sent Jesus Christ to die on the cross, but He also gave us the Holy Spirit for sanctification. So God's nature is love.

What do we do with our God who created us, and brought us salvation? Let us trust Him, accept Him, follow Him, and obey Him so that our end will be good.