Event Date: 
14-03-2022

Hivi karibuni, viongozi wa Umoja wa wanawake wakishirikiana na wanawake wote usharikani, walizindua mazao yatokanayo na mradi wa ufugaji wa nyuki.

Mradi huo ambao una jumla ya mizinga ipatayo arobaini, upo katika mtaa wa Tabora ambao unatunzwa na usharika wa Azania Front Cathedral,mradi huo umeweza kuwapatia mazao mengi yakiwemo asali, masega, juice na nta iliyoweza kutengeneza mishumaa. Mradi huo ni mradi endelevu ambao asali na mazao yake huvunwa kila baada ya miezi mitatu.

Viongozi wa Umoja wa wanawake usharikani, wakiwa madhabahuni Azania Front Cathedral kufanya uzinduzi wa  mradi wa asali na mazao yake .

--------------------------------------------------------------

Ripoti hii imeandaliwa na Jane Mhina