Date: 
20-09-2022
Reading: 
Mithali 3:9-10

Jumanne asubuhi tarehe 20.09.2022

Mithali 3:9-10

[9]Mheshimu BWANA kwa mali yako, 

Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.

[10]Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, 

Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

Uwakili wetu kwa Mungu;

Mali inaweka kutumika kama ishara ya kumheshimu Mungu pale inapotolewa kwa kazi yake. Ni pale inapotolewa kwake na mwenye mali husika. Yaani mkristo anapotoa mali yake kwa Mungu ni ishara ya heshima kwake Mungu aliyempa mali hiyo. Kumbe heshima kwa Mungu siyo maneno tu, ni matendo. Tendo hili la kutoa mali kwa Mungu linaanzia moyoni. Moyo ukiwa kwa Bwana ni rahisi kumtolea.

Utoaji wetu ni kipimo cha heshima yetu kwa Mungu. Tusipomtolea Mungu tunakuwa hatujamheshimu. Yeye ndiye muumbaji, atupaye afya na nguvu ya kutenda kazi. Lakini zaidi, sisi ni mawakili tu wa mali ambazo ni za Mungu. Hivyo tukimtolea Mungu tunampa mali yake, tunamheshimu.

Unamheshimu Mungu kwa mali yako?

Siku njema.