Date: 
20-02-2017
Reading: 
Matthew 10:1-15 (NIV)

MONDAY 20TH FEBRUARY 2017 MORNING                                

Matthew 10:1-15 New International Version (NIV)

Jesus Sends Out the Twelve

1 Jesus called his twelve disciples to him and gave them authority to drive out impure spirits and to heal every disease and sickness.

These are the names of the twelve apostles: first, Simon (who is called Peter) and his brother Andrew; James son of Zebedee, and his brother John; Philip and Bartholomew; Thomas and Matthew the tax collector; James son of Alphaeus, and Thaddaeus; Simon the Zealot and Judas Iscariot, who betrayed him.

These twelve Jesus sent out with the following instructions: “Do not go among the Gentiles or enter any town of the Samaritans. Go rather to the lost sheep of Israel. As you go, proclaim this message: ‘The kingdom of heaven has come near.’ Heal the sick, raise the dead, cleanse those who have leprosy,[a] drive out demons. Freely you have received; freely give.

“Do not get any gold or silver or copper to take with you in your belts—10 no bag for the journey or extra shirt or sandals or a staff, for the worker is worth his keep. 11 Whatever town or village you enter, search there for some worthy person and stay at their house until you leave.12 As you enter the home, give it your greeting. 13 If the home is deserving, let your peace rest on it; if it is not, let your peace return to you. 14 If anyone will not welcome you or listen to your words, leave that home or town and shake the dust off your feet. 15 Truly I tell you, it will be more bearable for Sodom and Gomorrah on the day of judgment than for that town.

Footnotes:

  1. Matthew 10:8 The Greek word traditionally translated leprosy was used for various diseases affecting the skin

Jesus sent His Apostles out in twos to preach and teach and heal the sick. Here he is giving them advice about what to do. Jesus was training the Apostles so that they could continue His work after He returned to heaven.

Thank God for those who today continue the work of building God’s church here on earth. Ask God to show you what part He wants you to play in this work.

JUMATATU TAREHE 20 FEBRUARI 2017 ASUBUHI                            

MATHAYO 10:1-15

1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 
2 Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 
3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; 
4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti. 
5 Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. 
6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 
7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; 
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake. 
11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka. 
12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. 
13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 
14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 
15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.
 

Yesu alituma Mitume wawili wawili kuhubiri injili na kuponya wagonjwa. Hapa anawapa maelekezo kabla ya kwenda. Yesu aliwafunza mitume kuendeleza kazi yake hapa duniani baada ya yeye kurudi mbinguni.

Mshukuru Mungu kwamba alikuwa na watumishi wake kuhubiri injili katika kila kizazi. Mshukuru Mungu kwa Watumishi wake wa siku hizi na waombee. Omba Mungu pia akuonyeshe wewe una nafasi gani katika kujenga Ufalme wa Mungu hapa duniani.