Date: 
29-01-2022
Reading: 
Matendo ya Mitume 10:9-16

Jumamosi asubuhi tarehe 29.01.2022

Matendo ya Mitume 10:9-16

9 Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.
14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.
15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
16 Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.

Mungu anaondoa ubaguzi;

Petro anapanda darini kusali, ndipo anapewa maono kuhusu  chakula, yeye akikiona chakula hicho  najisi. Anapewa ujumbe kuwa chakula kile  siyo najisi, kimetakaswa na Mungu. Petro anapewa rejeo la fundisho la Yesu kuhusu chakula;
Marko 7:15  Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.

Chakula hakiwezi kumtia mtu unajisi, bali mawazo yasababishayo maneno na matendo mabaya. Hivyo tunakumbushwa kuwaza vizuri,  ili tunene na kutenda vizuri kwa utukufu wa Mungu.

Kila kilichowekwa na Mungu kimetakaswa, hivyo tukitumie kwa utukufu wake. Lakini zaidi tuwe makini na mawazo, maneno na matendo yetu katika kuutafuta ufalme wa Mungu ulioandaliwa kwa ajili yetu.

Siku njema.